Shamsa Ford adhamiria kubadilika kimavazi

0
59

Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amedai kuwa mwaka huu ni mwaka wake wa kustaafu kuvaa nguo za vimini kwani amedhamiria kuwa mwanamke mwenye stara.

Shamsa alisema anamshukuru Mungu kuuona mwaka huu akiwa mzima na kwa kuwa mwaka mpya unakuwa na mambo mapya, yeye ameamua kubadilika katika suala la mavazi.

Amesema kuwa “Sina sababu tena ya kuendelea kutojistiri kwa sababu Mungu ameniokoa na kunistiri kwa kunipa mume, mwaka huu ni wa kuonesha kuwa mimi ni mama mwenye stara.

Pia amesema kuwa  anaamini kwa kuwa na duka la madira na mitandio ataweza kuwa mwanamke mwenye stara na hii ndiyo njia pekee ya kunipa mwisho mwema hapa duniani.

Shamsa ni staa ambaye maisha yake yote amekuwa akipendelea kuvaa nguo fupi, jambo lililokuwa likimfanya wakati mwingine asemwe vibaya hasa ikichukuliwa kuwa ni mke wa mtu.

 

 

LEAVE A REPLY