Shambulio kambini: Wanajeshi 17 wauawa, 35 wajeruhiwa Mali

0
171
Gunmen Attack Hotel in Mali, 170 Hostages Taken

Watu waliokuwa na silaha za kivita wamevamia kambi ya jeshi la Mali iliyopo katikati ya mji wa Nampala wamewaua wanajeshi 17 na kuwajeruhi wengine 35 kwenye kambi hiyo na kisha kuchoma moto sehemu ya kambi hiyo.

Makundi mawili tofauti ya waasi yamedai kuhusika na shambulio hilo.

Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita ameitisha kikao cha usalama na waziri mkuu wan chi hiyo, waziri wa ulinzi na makamanda wa majeshi ya nchi hiyo baada ya kufahamishwa kuhusu mkasa huo.

Nchi ya Mali inakabiliwa na changamoto za kiusalama kutokana na kuwepo kwa makundi mbalimbali ya kijeshi yanayoipinga serikali ya nchi hiyo yakihusisha makundi ya kikabila na makundi ya wapiganaji wa msituni.

Moja ya makundi mapya yaliyoundwa hivi karibuni limesema linahusika na shambulio hilo na limedai kuwa limeishambulia kambi hiyo ikiwa ni kulipiza kisasi kutokana na jeshi la Mali kulishambulia kundi la kabila la Fulani.

Kundi jengine la Ansar Dine pia limesema linahusika na shambulio hilo.

LEAVE A REPLY