Shahidi adai kukuta kipande cha sigara na siyo bangi wakati wa upekuzi wa nyumba ya Wema

0
110

Mjumbe wa Shina Namba 39, nyumbani anakoishi muigizaji wa Bongo Movie, Sepetu, Steven Alphonce ambaye ni shahidi katika kesi inayomkabili staa huyo, amedai wakati wa upekuzi walikuta kipande cha sigara wala si bangi.

 

Alphonce amesema hayo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula.

 

Wakati akitoa ushahidi wake katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Wema na wenzake wawili na kusema alishiriki katika upekuzi nyumbani kwa Wema na kukuta kipande hicho cha sigara jikoni na chumbani kwa Wema anakohifadhi viatu na nguo.

 

Amedai kuwa bangi anaijua ikiwa shambani kwani aliwahi kuiona Shinyanga lakini ikiwa nje ya hapo hawezi kuitambua. Wema na wenzake wawili wanashtakiwa kwa kutumia dawa za kulevya aina ya bangi na walikamatwa Februari 4, mwaka jana.

LEAVE A REPLY