Shahada ya mke wa Mugabe, Bi Grace Mugabe kuchunguzwa

0
127

Mamlaka ya kukabiliana na ufisadi nchini Zimbabwe imeanzisha uchunguzi kuhusu shahada ya udaktari iliopewa mkewe Robert Mugabe, Grace Mugabe.

Phyllis Chikundura ,msemaji wa tume ya kukabiiana na ufisadi nchini humo alithibitisha kuwa kulikuwa na uchunguzi uliokuwa ukiendelea.

Gazeti la serikali The Herald liliripoti wakati huo kwamba kutoweka kwa Bi Mugabe kulifanywa kwa lengo la kubadilisha hali ya jamii na kazi ya familia.

Bi Mugabe yeye mwenyewe alituzwa shahada hiyo na aliyekuwa rais wa taifa hilo Robert Mugabe ambaye alikuwa chansela wa chuo kikuu cha Zimbabwe.

Bi Mugabe alitumai kumrithi mumewe kama kiongozi, lakini akachokoza upande mmoja wa chama cha Zanu-Pf ambacho hatua iliosababisha mgawanyiko ndani ya chama hicho.

Jeshi baadaye lilingilia kati na kumlazimisha rais Mugabe kuondoka madarakani baada ya kipindi cha miaka 37 na kumuweka mamlakani aliyekuwa makamu wake Emmerson Mnangagwa kuwa rais.

LEAVE A REPLY