Serikali yaomba mkopo wa Dola Mil 150

0
126

Waziri wa Fedha na Mipango nchini, Dk. Philip Mpango ameiomba Benki ya Dunia (WB), kuipa Tanzania mkopo wa Dola 150 milioni za Marekani ili kuchochea ukuaji wa uchumi na utoaji wa huduma nchini.

Dk Mpango ametoa ombi hilo leo alipokutana na Mkurugenzi wa Uchumi Mpana, Biashara na Uwekezaji wa Benki ya Dunia, Felipe Jaramilo katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Mpango alifanikiwa kuelezea Mkurugenzi huyo namna Uvhumi wa Tanzania unapanda.

Aidha Waziri Mpango ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania haswa hii iliyopo madarakani katika kutekeleza miradi ya maedeleo nchini.

Dk Mpango ameeleza kuwa uchumi wa nchi umeendelea kukua kwa kiwango cha kati ya asilimia sita hadi saba kwa mwaka na hivyo kuiwezesha Serikali kuendelea na utoaji wa huduma za jamii na kuwekeza katika miradi ya maendeleo.

LEAVE A REPLY