Serikali ya Nigeria ‘yafuta’ mpango wa kujenga kijiji cha wasanii

0
192
Serikali ya Nigeria imefuta mpango wake wa kujenga kijiji cha wasanii kwenye jimbo la kaskazini mwa nchi hiyo la Kano kufuatia kupingwa vikali na mhadhiri wa kiislam pamoja na watu kupitia mitandao ya jamii.
Mradi huo wa kijiji cha wasanii ambao ulitengewa zaidi ya $10m (TZS 2bn) ulipangwa kujenga majumba ya kisasa kwaajili ya kuinua soko la filamu za kihausa unaofahamika kama Kannywood.
Serikali ya Nigeria ilieleza kuwa mradi huo ungesaidia kukuza utamaduni wa taifa hilo pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi wa taifa hilo lakini mhadhiri wa Kiislam aliyeupinga amedai kuwa mradi huo utaongeza uasherati na ukosefu wa maadili.
Pia, wananchi wengi wa Nigeria wametumia mitandao ya kijamii kuukataa mradi huo na kuitaka serikali ya Buhari kuusitisha.
Wananchi hao wamedai kuwa mradi huo haupaswi kuwa kipaumbele na badala yake serikali iwekeze nguvu kwenye kuyafufua mabwawa yaliyokufa ili kuinua kilimo kwenye nchi hiyo.
Mshauri wa rais Buhari, Abdurrahaman Kawu Sumaila, ametangaza kuwa serikali ya nchi hiyo imeyasikia matakwa ya wananchi na hawana budi kuyatii.

LEAVE A REPLY