Serengeti Boys inashuka dimbani dhidi ya Niger leo

0
220

Serengeti Boys leo inashuka dimbani dhidi ya Niger kwenye mechi ya raundi ya tatu ya mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17.

Katika mechi hiyo Serengeti Boys inahitaji kupata ushindi ili kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali na kukata tiketi ya kushiriki fainali za michuano ya Kombe la Dunia zitakazofanyika India Oktoba mwaka huu.

Serengeti Boys wenye pointi nne baada ya kuwafunga Angola mabao 2-1 matokeo ambayo Mali pia iliyapata dhidi ya Niger.

Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime alisema jana kuwa wachezaji wake wako vizuri na wamejipanga kumaliza na ushindi ili kutimiza ndoto.

LEAVE A REPLY