Scorpion ahukumiwa jela miaka saba

0
193

Mahakama ya Wilaya ya Ilala leo imemhukumu Salum Njwete ‘Scorpion‘ miaka 7 jela kwa kosa la kumjeruhi na kumtoboa macho Said Mrisho.

Pia mahakama hiyo imemtaka mtuhumiwa huyo kulipa faini ya TSH. Milioni 30 kwa ajili ya fidia kwa majeruhi huyo.

Lakini kwa upande wa mlalamikaji amedai adhabu hiyo haitoshi kwa mtuhumiwa baada ya kumtoboa macho.

Scorpion alikuwa anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni  unyang’anyi wa kutumia silaha na kumjeruhi Said Mrisho kwa kumchoma kisu sehemu mbalimbali za mwili zikiwemo, tumboni na mabegani na kisha kumtoboa macho kitendo anachodaiwa kutenda Septemba 6, mwaka juzi  katika eneo  la Buguruni Sheli, jijini Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY