Schweinsteiger ajiunga na klabu ya Chicago Fire ya Marekani

0
128

Kiungo wa Manchester United, Bastian Schweinsteiger amejiunga na klabu ya ligi kuu ya soka nchini Marekani, Chicago Fir.

Kiungo huyo, aliyekuwa hana nafasi kwenye klabu ya Manchester Uinted, tangu kutua kwa kocha Jose Mourinho msimu huu amekuwa akifuatiliwa na kocha wa Fire, Veljko Paunovic tangu mwezi Novemba.

 

Schweinsteiger amesaini mkataba wa mwaka mmoja na anatarajiwa kujiunga na klabu hiyo mapema wiki ijayo kutegemea upatikanaji wa Visa ya kuingia Marekani na kufuzu kwa vipimo vya Afya.

 

Nahodha huyo wa zamani wa Ujerumani amecheza mechi tatu tu za Manchester, United, tangu aje Mourinho majira ya kiangazi yaliyopita huku mechi yake mwisho ikiwa Februari 22 dhidi ya Saint-Etienne kwenye michuano ya Europa akiingia kutokea benchi.