Schwarzenegger achoka kukaa ndani

0
133

Staa wa filamu nchini Marekani, Arnold Schwarzenegger ameweka wazi kuwa amechoka kukaa ndani kama mfungwa tangu alipofanyiwa upasuaji wa moyo.

Schwarzenegger, mwenye umri wa miaka 70, alikuwa anasumbuliwa na tatizo la moyo na baada ya kufanyiwa upasuaji Machi 29, amekuwa mtu wa kukaa ndani.

Staa huyo sasa amedai kuwa amechoka na ameamua kutembea mitaani kukutana na mashabiki zake ili apunguze machungu.

“Nina furaha kuona nipo kwenye afya nzuri, mimi si mfungwa ambaye ninaweza kukaa ndani kwa kipindi kirefu, hivyo kutokana na hali yangu kuwa sawa nimeona bora nitembee mitaani kukutana na mashabiki.

“Najua mashabiki walikuwa wanatamani kukutana na mimi, hivyo nataka kuwaambia kuwa nipo sawa na nina furahi kuwaona na ninashukuru kwa salamu zao za pole,’.

LEAVE A REPLY