Samsung yakiri kuwa betri ndio chanzo cha kuungua kwa Galaxy Note 7

0
153

Kampuni ya Samsung imetoa matokeo ya utafiti wa sababu zilizokuwa zikisababisha simu zao za Galaxy Note 7 kupata joto kupita kiasi na kuungua.

Kampuni hiyo imedai kuwa software na hardware za simu hizo hazina matatizo kabisa lakini chanzo cha moto huo kilikuwa ni betri za simu hizo.

Samsung waliokuwa wakizishindanisha simu hizo na simu za iPhone, walisitisha utengenezaji wa simu hizo mwezi Oktoba mwaka jana kufuatia hatua ya kwanza ya kuzikusanya na kuzirudisha kiwandani simu zote zilizokuwa zimeshauzwa kwenye nchi mbalimbali.

Hatua hiyo ya ukusanywaji na urudishwaji kiwandani kwa simu hizo unadhaniwa kuigharimu kampuni hyo kiasi cha $5.3bn (TZS 12tn) na iliharibu sana heshima na hadhi ya kampuni hiyo kutoka Korea Kusini.

Uchunguzi wa ndani na uchunguzi mwingine huru wa chanzo cha kuungua kwa simu hizo kwa pamoja umethibitisha kuwa betri ndizo zilizokuwa chanzo cha kuungua kwa simu hizo.

Kampuni hiyo ambayo ilikuwa inaagiza betri za simu hizo kutoka kwenye kampuni mbili tofauti imedai kuwa haitofungua madai wala malalamiko yoyote dhidi ya kampuni hizo kwakuwa zilizkuwa zinafuata maelekzo ya mahitaji ya betri kwa mujibu wa matakwa ya Samsung.

Galaxy Note 7 zilizinduliwa Agosti 2016 kabla ya mwezi Septemba kampuni ya Samsung kuanza kuzikusanya simu hizo baada ya ripoti za kupata joto na kuungua ambapo simu milioni 2.5 zilikusanywa.

screen-shot-2017-01-23-at-11-11-18

screen-shot-2017-01-23-at-11-11-38

LEAVE A REPLY