Samatta na Mkwasa walivyopishana ‘falsafa’ tuzo za FIFA 2016

0
646

Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars Charles Mkwassa na aliyekuwa nahodha wa kikosi cake Mbwana Samatta wameonyesha kuwa ingawa wote walikuwa wakifanya kazi pamoja kwenye kikosi cha Taifa Stars lakini walikuwa na falsafa zinazotofautiana.

Wawili hao wakati bado wakiwa na majukumu ya kuitumikia timu ya taifa walikuwa na nafasi ya kupiga kura kuchagua washing wa tuzo za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa upande wa wachezaji bora na makocha bora.

Mattock ya kura zao yamedhihirisha wazi kuwa mitazamo ya wawili hao katika soka ‘haifanani’ ingawa inaweza kuwa kura hizo zilikuwa na ushawishi wa mapenzi binafsi kwa wachezaji, makocha au vilabu wanavyotokea.

Hebu tazama kura zao na matokeo ya mwisho ya FIFA.

Tuzo ya Mchezaji bora (Wanaume):

Mbwana Samatta: Lionel Messi

Charles Mkwassa: Cristiano Ronaldo

Mshindi wa FIFA: Cristiano Ronaldo

mkwasa-kwa-wachezaji

samatta-tuzo-za-fifa

Tuzo ya Kocha bora (Wanaume):

Mbwana Samatta: Luis Enrique

Charles Mkwassa: Klopp Jurgen

Mshindi wa FIFA: Claudio Ranieri

mbwana-kocha-bora

mkwasa-kura-kwa-kocha-bora

LEAVE A REPLY