Samatta aendelea vizuri baada ya kuumia goti

1
372

Mshambuliji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amesema kwamba sasa anajisikia vizuri na ameanza mazoezi mepesi baada ya kupata ahueni ya maumivu ya goti.

Samatta aliyeumia katika mchezo wa kwanza wa Kundi F Europa League dhidi ya Rapid Viena Alhamisi iliyopita Uwanja wa Allianz, Viena, Austria, KRG Genk ikifungwa 3-2 amesema anaendelea vizuri.

Samatta amekosa mechi moja ya Ligi ya Ubelgiji wakifungwa 2-0 na Anderlecht Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk Jumapili na jana katika kombe la Ligi ya Ubelgiji, wakishinda 4-0 ugenini dhidi ya Eendracht Aalst Uwanja wa Het Pierre Cornelisstadion.

Tangu amejiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, Samatta amecheza jumla ya mechi 25 za mashindano yote 18 msimu uliopita na saba msimu huu akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY