Sam wa Ukweli adai kufuatwa na mastaa wa kike kutengeza kiki

0
409

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Sam Wa Ukweli amefunguka na kudai kuwa amefuatwa na baadhi ya mastaa wa kike Bongo kwa ajili ya kutengeza kiki lakini amekataa suala hilo.

Sam wa Ukweli amesema hayo baada ya kuulizwa kama anafuatwa na baadhi ya mastaa wa Bongo wa kike ili kufanya ‘kiki’.

Amesema kuwa ‘Ni kawaida yangu kutafutwa na mastaa mbali mbali wa kike wakitaka wafanye matukio watafute kiki’.

Sam Wa Ukweli kwasasa amerudi ramsi kwenye game baada ya kutambulisha nyimbo yake mpya baada ya kupumzika kwa kipindi kirefu.

Pia mwanamuziki huyo amesema kuwa aliyekuwa meneja wake ‘Maneno’ kudai kuwa wakati wanafanya kazi wote Sam alikuwa anaenda sana kwa waganga ili muziki wake ufanye vizuri kauli ambayo Sam amedai pia ilikuwa yakutafuta kiki.

LEAVE A REPLY