SALOME ya Diamond ndio ngoma kubwa zaidi kwa Video queens?

1
787

Hakuna asiyejua kuwa Diamond Platnumz alipata haki ya kutengeneza tena ngoma ya staa wa zamani wa muziki wa asili Saida Karoli, SALOME kisha akaitendea haki kwenye video ya gaharama kubwa.

Ukweli mwingine ni kuwa Diamond aliwatumia warembo ‘ghali’ Tanzania kwenye video hiyo ili kupata kazi bora zaidi ya zilizotangulia. Lakini je, warembo waliopo kwenye nyimbo hiyo wanapaswa ‘kuithamini’ video hiyo?

Licha ya mrembo Tunda kutamka kauli isiyo ya kiungwana dhidi ya Diamond Platnumz hususani kuhusu kazi ya SALOME ambayo yeye ameshiriki kama ‘model’ lakini hizi ni sababu za warembo walioshiriki kazi hiyo kuzingatia hususani kwenye kusaka kazi nyingi zaidi:

Views YOUTUBE: 9.2m

Endapo hakuna udanganyifu wa kununua views basi warembo waliopo humo huenda wakanufaika zaidi kwa kazi hiyo

Diamond Platnumz as a brand

Hakuna msanii wa Afrika mwenye jina kubwa asiyemfahamu Diamond na wengi wanafuatilia kazi zake hivyo huenda hilo likawasaidia kuwaunganisha warembo hao na wasanii wa kimataifa.

Saida Kalori na umaarufu wa Salome ‘remix’

Mmoja wa mastaa wa muziki wa asili kutoka Tanzania aliyewahi kutingisha Afrika Mashariki na kati kwa kazi zake, ni wazi kuwa mashabiki wake wengi wangependa kuona toleo la pili la kazi hiyo. Hivyo, hiyo itawapa nafasi ‘warembo hao’

Ziara za Diamond kimataifa

Anapiga shoo Afrika, Marekani na Ulaya hivyo haitakuwa ngumu kwake kuwaonyesha watu video hiyo na kuwaunganisha video queens wake na masoko ya kimataifa.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY