Sallam SK adaiwa kujitoa WCB

0
127

Meneja wa Diamond Platnumz’, Sallam SK ameibua utata mpya wa kudaiwa kujitoa kwenye lebo hiyo licha ya mwenyewe kutokiri suala hilo.

Hii sio mara ya kwanza kwa tetesi kuzagaa kuwa, meneja huyu amejitoa kwenye lebo hiyo, miezi kadhaa iliyopita, taarifa hizo zilisambaa na kulifikia gazeti hili lakini alipoulizwa Sallam alikataa kusema ukweli.

Habari zimesema kuwa Sallam ameshajitoa kwenye lebo hiyo japo wenyewe wameamua kufanya siri ili kuepuka kuwavuruga mashabiki.

“Hawataki kuwachanganya mashabiki kwa habari hiyo ndio maana unaona wameamua kukaa kimya. Na hata ukiwauliza, wote watakwambia tu wapo sawa kumbe kiuhalisia hawako sawa, kila mtu ana maisha yake,” kilisema chanzo hicho.

Sallam kwa sasa yupo bize na miradi yake binafsi ikiwemo online televisheni pamoja na redio yake iliyopo mkoani Morogoro.

Sallam amekuwa haonekani kwenye matukio ya Wasafi ikiwemo lile muhimu lililowakusanya mameneja wote wa Diamond hivi karibuni.

LEAVE A REPLY