Salam SK amlipua Harmonize

0
35

Meneja wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz aitwae Salam SK amefunguka na kuandika ujumbe wa kebehi kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya Rayvanny kuwekwa rumande.

Ujumbe unahisiwa kumlenga mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ambaye ndiyo alikuwa kituo cha Polisi pamoja Kajala kuhusu mwanamuziki Rayvanny kusambaza picha akiwa na mtoto wa Kajala.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram ameandika- Kuna Panya mmoja amekesha kituo cha polisi kulazimisha msanii mwenzie awekwe ndani lakini kutokana na sheria ya nchi haipo mkononi mwake, ikabidi akimbilie kwenye media kujifanya anaomba suluhu.

Yeye anataka amani na anamuombea asipate matatizo, Huyo Panya anahangaika ili msanii mwenzie apate matatizo.

Nikupe taarifa NDUGU PANYA dua zako wala maombi yako hatuyahitaji labda uyapeleke Hospital kufanikisha kizazi chako kiwe bora na uweze kulea mtoto wako binafsi na sio mtoto wa kukodi.

 

LEAVE A REPLY