Salam Sk adai kuna njama za kumshusha Diamond kimuziki

0
358

Meneja wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Sallam SK amedai kwamba kuna watu wanataka kumshusha msanii huyo ambaye anafanya vizuri kwasasa.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Sallam ameandika kuwa kuna baadhi ya watu wanataka kumshusha Diamond kwenye ramani ya muziki nchini suala ambali kwake amesema itakuwa ni vigumu sana.

Licha ya Salaam kuandika madai hayo lakini hawajewaka bayana ni nani wana nia ya kumshusaha mwanamuziki huyo kutoka lebo ya WCB.

Kwenye akaunti yake ya Instagram ameanza kwa kuandika  “Kumbe tatizo ni kumpoteza huyu kijana?(Diamond) Waambie familia yako na wazazi waliyokuleta katika haya maisha huyu mtoto kaletwa kwa makusudi maisha haya, ili kuleta ukombozi wa dhuluma uliyokuwa unaleta kwenye Taifa hili, unatakiwa kujua Kwanza hili Taifa sasa Rais anaitwa John Pombe Magufuli,”.

Inasemekana kuwa  wasanii wa WCB kwasasa hawapati airtime kama kipindi cha nyuma hali ambayo inatishia kazi yao ya muziki.

LEAVE A REPLY