Sakaya adai hawezi kuhama CUF licha migogoro

0
83

Naibu Katibu wa CUF Tanzania Bara, Magdalena Sakaya  amesema kuwa hawezi kuhama Chama hicho na iwapo na ikitokea Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ikiamua kukifuta atastaafu siasa.

Sakaya amesea kwamba Mgogoro unaoendelea ndani ya chama chao ni wa Kikatiba na unafahamika kwa msajili wa vyama na kuongeza kama ikitokea kwamba CUF inafutwa basi yeye atastaafu siasa na siyo kuhama chama.

Amesema kuwa “Kwanza naamini CUF haiwezi kufutwa. Yaani hilo halipo pamoja na changamoto ya mgogoro iliyopo. CUF ina misingi yake na mgogoro uliopo ndani yake ni wa kikatiba. Kwa hiyo, mimi nikiamua kwamba sasa sitaki kuendelea kuwapo CUF, ninaacha siasa. Ninaendelea na mambo yangu mengine, eeeh”.

Pia Sakaya amesema kuwa amesema kuwa “Kwanza mimi sijawahi kuwa na kadi ya CUF pekee. Nakumbuka wakati tunaripoti Shule yaSekondari ya Wasichana Kibosho (mwaka 1986) tuligawiwa kadi za kijani (CCM) wakati ule nchini kulikuwa na chama kimoja. Baadaye nikiwa na akili yangu timamu kadi niliyoichukua ni ya CUF ambayo niliichukua mwaka 1995 na ninayo mpaka leo na nitaendelea kuwa nayo.

LEAVE A REPLY