Sababu ya Wolper kuuza gari yake

0
106

Muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Massawe maarufu kama Wolper amefunguka na kuweka wazi kuwa Hivi karibuni alifikia uamuzi wa kuuza gari lake.

Wolper ambaye alikuwa anamiliki gari aina ya Toyota Brevis, ameweka wazi kuwa ameamua kuuza gari lake hilo ambalo lilikuwa ndio Usafiri wake pekee ili anunue matirio za kutengenezea magauni.

Wolper ameweka wazi kuwa aliamua kuchukua uamuzi wake huo baada ya kupendezwa na matirio hayo alipokuwa nchini Dubai hivi karibuni.

Amesema kuwa Unajua mimi ni fundi cherehani hivyo  nilivyofika nchini Dubai na kuwaona wadada wakipendeza kwa kuvaa magauni kama haya na nilipowaangalia niliona kabisa kuwa nayamudu kuyadizaini.

Pia amesema kuwa Nilichoamua kufanya ni kuuza gari yangu na kwenda kununua matirio haya na kutengeneza magauni kadhaa ambayo kama hili na mengine nayauza. Kwa sasa natumia usafiri wa kukodi na hilo kwangu sioni shida”.

LEAVE A REPLY