Sababu ya Wolper kudondoka mkoani Mwanza

0
101

Muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amejikuta akipata fedheha ya aina yake baada ya kuanguka mbele za watu mkoani mwanza alipoudhuria Tamasha la Wasafi Festival.

Wolper alianguka kwenye ufukwe wa Jembe ni Jembe jijini Mwanza wakati wa pati ya awali ya onesho lao la Wasafi Festival lililofanyika katika Uwanja wa CCM-Kirumba.

Ulipofika wakati wa Wolper, yeye aliamua kupanda juu ya meza kama wafanyavyo wanenguaji wa staili ya kusasambua.

Akiwa juu ya meza, DJ aliweka Wimbo wa Kwangwaru ambapo Wolper aliendelea kuonesha umahiri wa kukicheza kwa kukata mauno baab’kubwa. Kwa bahati mbaya, wakati akiendelea kufanya yake, maskini mwanadada huyo mrembo alipiga mwereka matata na kuangukia kisogoni.

Wolper alisaidiwa kunyanyuka na mabaunsa na mashabiki waliokuwa karibu ambao walimuinua kisha wakamkagua na kubaini hakupata maumivu makali hivyo shoo yake ikaishia hapo.

LEAVE A REPLY