Sababu ya Vanessa Mdee kuacha mziki

0
67

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amefunguka na kusema hataki kuwa sehemu ya tasnia ya muziki na mfumo wa kazi wala kwenye soko la muziki.

Vanessa amehusisha sababu kama ulevi uliopitiliza, ugomvi na mama yake,sapoti huzuni na presha ndiyo vimemfanya kuacha muziki.

Msanii huyo ameweka wazi suala hilo la kuacha muziki kupitia YouTube Channel yake Vanessa Mdee.

“Nimepitia changamoto nyingi sana kwenye upande wa muziki na imenipelekea kutaka kuacha au kuamua kuacha kuwa sehemu ya soko la muziki.

Pia amesema kuwa nyuma ya pazia tasnia ya muziki ni tasnia ambayo bila ya kufahamu au kuielewa vizuri unaweza ukaona tunafanya show, tunasafiri, tunaachia nyimbo tuna mashabiki lakini kiukweli sio sehemu ya kawaida ya maisha ya mwanadamu”.

Vanessa Mdee amesema alikuwa na ugomvi na mama yake kuhusu muziki hali iliyokuwa akikosa sapoti kutoka kwa mzazi wake huyo, pia ulevi, huzuni na presha vimechangia kuacha muziki.

LEAVE A REPLY