Sababu ya Vanessa Mdee kuacha muziki

0
140

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa mdee ni miongoni mwa wanamuziki maarufu wa kike nchini Tanzania na barani Afrika.

Siku kadhaa zilizopita Mdee alitangaza kuacha shughuli zote za muziki na burudani kupitia Podcast yake inayoitwa ‘Deep dive with Vanessa Mdee’

Katika maelezo yake anasema amekua akikabiliana na msongo wa mawazo kwa muda mrefu kutokana na shughuli za muziki.

”Nimekua nikiishi kwa nje najificha lakini ndani nakufa, nilikuwa siwezi kulala hadi ninywe pombe”

”Sina hamu tena ya kufanya muziki, sina hamu tena ya kuhudhuria shughuli yoyote ya kupokea tuzo, kuanzia sasa sitajihusisha tena, hapana, ni msongo wa mawazo, ni shinikizi kubwa” anasema Vanessa.

Aidha katika mambo ambayoo amesema yamesababisha kuwa na msongo wa mawazo kwenye tansia ya muziki, ni jinsi ambavyo anatakiwa kuishi Maisha Fulani kila siku ambayo si ya kweli kwake yeye binafsi na matakwa yake.

Vanessa ameongeza pia gharama za kuendesha shughuli ya muziki zilikua kubwa kuliko faida yake.

”Nafanya show kwa dola 1000 , hapo unatakiwa kutoa gharama ya kila kitu, kuwalipa watu, mimi mwenyewe, se

Vanessa Amefikia uamuzi huu baada ya kuwa katika tasnia ya muziki kwa zaidi ya miaka 10.

Anasema kila mwaka amekua akirudia mfumo wa Maisha huo huo, amekua akiridhisha wengine lakini hakua na furaha yeye binafsi.

”Nimekua nikiridhisha watu wengine kila siku kwa miaka 13, nimekua kwenye muziki kwa miaka saba, lakini nimeanza kujihusiha zaidi ya miaka 13, na kila siku hali ni ile ile”.

Baada ya kutoa maamuzi yake Vanessa anasema amepata ujumbe wa wasanii mbalimbali wakimwambia amefanya uamuazi mzuri, na baadhi wanapitia hali kama yake lakini hawajapata ujasiri wa kuweka wazi.

 

LEAVE A REPLY