Sababu ya Shamsa Ford kutojichanganya na wenzake

0
284

Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amefunguka sababu inayompekea kutoonekana kwenye matukio mbalimbali ya wasanii wenzake.

Shamsa Ford kwa sasa amekuwa haonekani akijichanganya na wenzake jambo ambalo limezua minong’ono na kusababisha mwenyewe kuibuka na kudai kuwa amekatazwa na mume wake Chid Mapenzi.

Muigizaji amesema kuwa, awali alikuwa akijichanganya mno kwenye ishu tofauti lakini kwa sasa anashindwa kutokana na kupigwa marufuku na mumewe, Chid Mapenzi, baada ya kuwa na ujauzito mchanga ambao ulichoropoka kwa sababu ya kuzurura.

Amesema kuwa “Nilipigwa marufuku kutokatoka licha ya kwamba mwanzoni nilikuwa ninatoka kibishibishi tu, lakini kwa sasa imenibidi nimsikilize mume wangu zaidi maana mimba changa ilitoka kwa sababu ya kutokatoka hovyo kwenda kwenye shughuli,”.

Muigizaji huyo kwasasa ni mke wa mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Chid Mapenzi ambaye ameamua kumpiga marufuku mke wake huyo.

LEAVE A REPLY