Sababu ya Salam SK kukataa mkono wa Harmonize

0
81

Meneja mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz, Sallam SK amefunguka sababu ya kutopokea mkono wa mwanamuziki Harmonize kwenye msiba wa mke wa meneja mwnezake Babu Tale.

Sallam amesema kuwa tofauti kati yake na Harmonize ilianza muda mrefu tangu miaka mitatu iliyopita, baada ya Harmonize kumtuhumu yeye na Babu Tale kuwa ndio waliopeleka taarifa kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwamba Harmonize anavuta bangi.

Sallam ameeleza kwamba tangu kipindi hicho, Harmonize hakuwahi kumsalimia na alikuwa akimpita kama jiwe mpaka siku ya msiba wa mke wa Babu Tale ambapo alimsalimia Sallam lakini naye aliukataa mkono wa msanii huyo.

“Mimi sio mnafiki, kama mtu aliamua kutonisalimia na mara nyingi amekuwa akinikataa kwa zaidi ya miaka mitatu sasa. kuna haja gani ya kusalimiana naye. Ndio maana hata ule mkono alionipa niliukata.

LEAVE A REPLY