Sababu ya Rosa Ree kuposti picha za Black & White

0
69

Mwanamuziki wa Hip Hop Tanzania Rosa Ree amewatolea ufafanuzi watu waliokuwa hawafahamu kuhusiana na Challenge inayoendelea sasa hivi mitandaoni ya kupost picha za Black&White

Rosa Ree ameandika kuwa “Jana nili post picha ya Black and White baada ya kuambiwa na marafiki zangu wakike, niwe mkweli nilikuwa sijui nini maana yake. Kwa kawaida chochote kinachohusu wanawake huwa nakiunga mkono lakini leo nimejua nini maana yake”

“Ushindani huu umeanzia Uturuki ambapo wanawake wamekuwa wakiuwawa na kesi nyingi hazichukuliwi hatua za kisheria.

Baada ya tukio kutokea jamii huamua kupost picha za White&Black na muuaji hukatwa kiganja au kuachiwa huru.

Pale tunapo post picha ya Black&White kama wanawake tunamaanisha kuwa zamu inafuata. Tuwaunge mkono wanawake wa Uturuki na kuwa na umoja kupigania haki za Binadamu. Tunawapenda sana”.

LEAVE A REPLY