Sababu ya Mwasiti kufanya nyimbo na wasanii wa kiume

0
32

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mwasiti Almasi amefunguka na kusema kuwa anapenda kuwashirikisha wanaume kwenye nyimbo zake kwasababu wapo serious kuliko wasanii wa kike.

Kauli ya mwanamuziki huyo imekuja baada ya kueleza kuwa wimbo wake wa Hao alioimba na Chid Benz alitakiwa kufanya na Profesa Jay lakini ikashindikana kutokana na Profesa Jay kuwa bize wakati huo.

Mwasiti amesema kuwa mipango ilikuwa ni kumshirikisha Prof Jay ila ikashindikana ndipo akatafutwa Chidi Benz.

Mwasiti ameeleza kwa nini hufanya kazi zaidi na wasanii wa kiume kuliko wasanii wa kike kwa kusema  “Watoto wa kiume wapo serios sana unapofanya nao kazi, hawawezi kukuangusha unapofanya nao kazi napenda sana watoto wa kiume kwa sababu hiyo, pili mimi napenda sana HipHop”.

Mwasiti ameshafanya kazi na wasanii wa kiume kama Chidi Benz, Ally Nipishe, Godzilla, Roma, Billnass na G Nako.

 

LEAVE A REPLY