Sababu ya Mobeto na Diamond kupima DNA

0
35

Mwanamitindo maarufu nchini, Hamisa Mobeto amethibitisha tetesi za mzazi mwenza wake Diamond Platnumz kuchukua vipimo vya DNA na mwanae Daylan.

Hamisa amesema kuwa waliamua kwenda kupima vipimo vya DNA baada ya maneno kuzidi kusambaa juu ya mtoto kuwa ni wa mwanamuziki Jagwa.

Hamisa Mobetto amesema kuwa ni kweli Diamond alifanya hivyo ili kujihakikishia na majibu yalitoka asilimia 100% mtoto huyo ni wakwake.

Hamisa amefunguka “Tulienda hospitali na tukachukuliwa vipimo vinne vinne, wakasema tusubirie wiki mbili au tatu na majibu yakatoka mtoto kwa asilimia zote 100% ni wakwake”.

Hamisa na Diamond Platnumz wamejaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwae Dalan mwenye umri wa miaka miwili.

LEAVE A REPLY