Sababu ya mme wa Amber Rutty kuanguka mahakamani

0
139

Video queen Bongo, Amber Rutty ameeleza sababu iliyopelekea mume wake, Said Mtopali kudondoka ghafla mahakamani kuwa ni kutokana na hali ya kizunguzungu aliyokuwa akijisikia.

Amber Rutty amesema kwamba hali ya mume wake haikuwa nzuri tangu walipotoka gereza la Segerea kwa kuwa walikubwa na maradhi.

Amber Rutty amesema kwamba kwa sasa mume wake ameshapatiwa huduma ya kwanza na tayari amepatiwa ‘drip’mbili za maji.

Hakimu Mkazi Kisutu, Janeth Mbando ameahirisha kesi inayowakabili wanandoa hao kwa kusambaza video chafu mitandaoni hadi Februari 11, 2019 baada ya Wakili Neema Mbwana kusema upelelezi haujakamilika.

Wanandoa hao wapya ambao wamefunga ndoa wiki iliyopita wamedai baada ya matatizo yao kwisha watafanya sherehe ili kusherehekea ndoa yao.

LEAVE A REPLY