Sababu ya Mabeste kufikishwa kituo cha Polisi

0
120

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mabeste amehojiwa katika kituo cha Polisi Oyster Bay kwa kosa la kumchafua mitandaoni mzazi mwenziye na mkewe wa zamani Lissa.

Mabeste amesema ameenda kituo cha Polisi na anasubiria hadi atakapopangiwa kwenda tena kwa kosa la kumchafua kupitia wimbo wake mpya wa Back Off.

Pia anashtumiwa kwa kosa la kumtangazia kwa watu na kwenye vyombo vya habari kwamba mtoto aliyekuwa naye sasa hivi ni wake.

Mabeste amesema kuwa “Ishu ni kwamba nilikuwa nimeshtakiwa na mzazi mwenzangu kwamba namdhalilisha, nimeenda kusikiliza malalamiko yake.

Mwanamuziki huyo ameongeza kwa kusema mke wake huyo wa zamani anadai kwamba amemchafua kwenye mitandao kupitia wimbo wa Back off.

Mabeste amesema kuwa mwanamke huyo anadai wimbo wake wa Back Off unamlenga yeye katika kumdhalilisha zaidi, kingine ni mtoto wake aliyempata sasa hivi, anadai natangaza kwamba ni wa kwangu kwa hiyo inamletea shida kwenye mahusiano yake.

LEAVE A REPLY