Sababu ya Kala Jeremiah kuachia wimbo wa ‘Wewe’

0
28

Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Kala Jeremiah amefunguka baada ya ndoa yake anayodai ni ya kideoni kushtua wadau wengi tofauti na alivyodhania.

 

Ngoma mpya ya Kala aliyomshirikisha Sholo Mwamba inayokwenda kwa jina la Wewe ambayo ndani yake anawapa somo akina dada wanaotarajia kuingia na waliopo kwenye ndoa.

 

Kala anabonga kwamba amefikiria hatua ya kutunga mashairi hayo baada ya kusikitishwa na janga la kuvunjika kwa ndoa nyingi kila kukicha.

 

Kala anasema katika mambo yanayomuumiza roho ni kusikia wanandoa au wachumba wameachana, hali iliyomsababisha kufikiria kisha kutunga mashairi ya ngoma hiyo ambayo anaamini kwa atakayeyasikiliza mashairi yake na kuyafanyika kazi, atakuwa ameinusuru ndoa yake.

Kala anasema; “Katika maisha yangu, ukweli ninaposikia wanandoa wameachana na pengine hata wakiwa wachumba, inaniuma sana kama mimi ndiye mhusika, huwa sipendi kabisa itokee hivyo.

 

Pia ameema kuwa “Hivyo baada ya kufikiria hilo, nimeona nitoe ngoma hii ambayo naamini kama atakayesikiliza vizuri ujumbe wake, atakuwa ameinusuru ndoa au uchumba wake.

LEAVE A REPLY