Sababu ya Kajala kumpeleka Harmonize Polisi

0
45

Muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja ameweka wazi sababu iliyomfanya kumpeleka kituo cha polisi msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize.

Kajala ameeleza kuwa kama kweli anamahusiano ya kimapenzi na msanii huyo basi kipindi cha nyuma wasingepelekana polisi. “Watu hata kujiongeza ni mtihani jamani!, “Kama tungekuwa wapenzi kwa nini tulipelekana hadi polisi kisa kuposti picha yangu kwenye mtandao.

Pia akaongeza “Hebu wafikirie huyu mtu wangu akisikia hivyo itakuwaje, hata kama hatayazingatia haya mambo ya mitandaoni lakini moyoni mwake huwezi kujua anawaza nini, vivyo hivyo kwa Harmo na huyo mpenzi wake.

Naomba watu watambue kuwa kila mmoja wetu yupo kwenye mahusiano yake ya kimapenzi. Sasa kuendelea kutuzushia kuwa tunatoka pamoja huko ni kuharibiana maisha kitu ambacho sio kitu kizuri kabisa. Waache kuharibu mahusiano ya watu.

LEAVE A REPLY