Sababu ya Jay-Z na Beyonce kusimama mbele ya picha ya Meghan Markle

0
147

Wanamuziki wa Marekani, Beyonce na Jay-Z wakiwa wamepiga picha mbele ya picha ya mwana mfalme akiwa amevalia taji baada ya kushinda tuzo ya kundi bora katika tuzo ya Brits.

Beyonce aliandika katika kurasa yake ya Facebook na kusema kuwa kwa heshima ya kihistoria ya watu weusi, tunatoa heshima kwa moja ya picha ambayo inatuwakilisha.”

Picha kama hiyo pia wanaifananisha na picha ya video ambayo walipiga wakiwa wamesimama mbele ya picha maarufu ya Monalisa huko Louvre, Paris.

Lakini katika tuzo za Brits, Wapenzi hao walipiga picha karibu na picha ya Meghan Markle.

Katika gazeti la Guardian, muhariri wa muziki Laura Snapes amesema uamuzi wa kukubali kupata tuzo yao mbele ya picha ya Meghan ilikuwa ni jambo zuri sana.

Watu wengine walipendekeza kwamba picha ya Beyonce na Jay Z ilikuwa ni ujumbe kwa vyombo vya habari kwa ajili ya kumuunga mkono Meghan.

Msanii aliyepiga picha ya Meghan , Tim O’Brien, alisema kwenye redio kuwa Meghan anaibadili taswira ya Uingereza na amekuwa ishara kuwa utawala wa watu weupe upo katika maendeo yote duniani.

Lakini anatuambia kuwa alibaini kuwa Beyonce na Jay Z ametumia mfano wa picha aliyomchora Meghan kama watu wengine tu walivyoona.

Mchoro huu uliagizwa kuchorwa kwa mara ya kwanza mwaka 2018 kwa ajili ya jarida linaloitwa ‘The key’.

 

LEAVE A REPLY