Sababu ya Grace Matata kuchia wimbo wake ‘Me and You’

0
25

Mwanamuziki wa Bongo Fleva,Grace Matata ameachia wimbo wake wa kwanza baada ya kimya cha muda mrefu ndani ya game ya Bongo Fleva.

Wimbo huo unakwenda kwa jina la ‘Me and You’ na ni miongoni mwa nyimbo nne (4) zinazopatikana kwenye EP project ya REBIRTH.

Kazi hiyo mpya imefanyika kwenye studio za Fisher Records zilizopo Kunduchi, Dar Es Salaam chini ya Mtayarishaji wa muziki Taz Goemi.

Grace alitamani awe na wimbo wa aina hii kwenye project yake mpya, wimbo fulani umechangamka lakini pia uwe soft kwenye masikio, wimbo ambao ukiwa sehemu na marafiki unaweza enjoy lakini ukiwa peke yako nyumbani pia utaweza uenjoy.

Grace amesema kuwa alihitaji wimbo wa kuchangamka ambao mtu akisikia aweze kuvutiwa na wimbo huo baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa EP yake hiyo inapatikana katika platform zote za kuuza nymbo hivyo mashabiki wake wanaweza kusikiliza kupitia platform hizo.

LEAVE A REPLY