Sababu ya DC Jokate kuanzisha ‘Tokemeza Zero’

0
27

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amefanikiwa kuvuna mamilioni ya fedha kwenye kampeni yake ya ‘Tokomeza Zero’ yenye lengo la kuchangia elimu wilayani humo.

DC Jokate miezi mitatu iliyopita alianzisha harambee ya kuchangia elimu kupitia kampeni hiyo ya Tokomeza Zero, ambapo alianzia kampeni wilayani humo na kufanikiwa kukusanya zaidi ya Tsh milioni 125.

Kwenye kampeni hiyo aliyoanzisha ikiwa ni miezi 6 tu iliyopita, DC Jokate ameonekana kuungwa mkono na viongozi mbalimbali Serikalini, Taasisi, Mashirika na wadau mbalimbali wa elimu.

Kampeni hiyo ya Tokomeza Zero ilianza kupata umaarufu kwenye mitandaoni ambapo watu wengi maarufu wakaanza kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Kampeni hiyo, haikuishia hapo tu Jokate akaipanga kwa ukubwa ambapo ambapo awamu hii aliifanyia katika Ukumbi wa Mlimani City wikiendi ilyopita ya Machi 31, 2019.

Kwenye harambee hiYO, Jokate alifanikiwa kwa kiasi chake kwani ilihudhuriwa na mamia ya watu wakiwemo viongozi wakuu serikali.

Hata hivyo DC Jokate ameahidi kutoa taarifa rasmi ya makusanyo yote ya harambee hiyo, mapema atakapomaliza mahesabu.

Kampeni ya Tokomeza Zero ilianzishwa na DC Jokate miezi takribani 6 ikiwa ni miezi mitatu tangu ateuliwe na Rais Magufuli mnamo July 28, 2018.

LEAVE A REPLY