Sababu ya Belle 9 kuimba gospel

0
27

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Belle 9 amesema ameamua kuimba wimbo wenye mahadhi ya gospel baada ya kujitafakari ndani ya nafsi yake kufuatia tukio la kupata ajali ya gari.

Belle 9 alipata ajali ya gari siku ya Septemba 7, akiwa na wasanii wengine ambao ni Bonge la Nyau na Lulu Diva na kupata baadhi ya maumivu kutokana na ajali hiyo.

Belle 9 amesema eneo hilo ambalo amepata ajali ni ngumu sana watu kusalimika ila yeye amefanikiwa kutoka salama ndiyo maana akaimba wimbo huo wa injili ili kumshukuru Mungu.

Amesema kuwa “Baada ya kupata ajali nilitumia muda mwingi kujitafakari ndani ya nafsi yangu, niliambiwa eneo nililopata ajali watu wengi huwa wanapotea kabisa, kwahiyo matokeo ya kuimba ule wimbo ni baada ya kutoka salama na kutoa shukrani, nimeujua ukubwa wa mungu na sasa hivi maisha yangu yamebadilika”.

Belle 9, Bonge la Nyau na Lulu Diva walipata ajali ya gari maeneo ya Chalinze wakati wanatoka kwenye kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ilolo, Mkoani Iringa.

LEAVE A REPLY