Sababu ya Aunty Ezekiel kuachana na wapenzi wake

0
161

Muigizaji wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel amesema moja ya kitu ambacho kinafanya mahusiano yake kuvunjika ni usaliti anaofanyiwa na mpenzi wake katika mahusiano.

Aunty Ezekiel, amesema kwenye mahusiano yoyote ambayo yanavunjika kila mtu huwa anakimbilia kusema yeye ndiyo amekosewa.

“Mahusiano yangu hayajawahi kuvunjika sana, tangu watu wamenifahamu yamevunjika mahusiano mangapi, ila mimi sipendagi usaliti, mtu akinisaliti mahusiano huwa siyawezi kabisa”.

Aidha msanii huyo wa filamu ameendelea kusema “Unajua katika mahusiano yoyote ambayo utamuuliza mtu atakwambia yeye ndiyo amekosewa, lakini mimi naamini katika mapenzi watu hukoseana ila mimi sijawahi kumsaliti mtu”.

LEAVE A REPLY