S2kizzy aweka wazi ilipofikia kesi yake ya kuvamiwa

0
49

Mtayarishaji wa muziki nchini, S2Kizzy amefunguka kinachoendelea kwenye kesi ya kuvamiwa na kushambuliwa studio kwake na watu waliojitambulisha kuwa ni sungusungu kwa kusema wapelelezi wanaendelea na uchunguzi pia kuna watuhumiwa tayari wameshakamatwa.

“Kila kitu kipo chini ya polisi kwa hiyo watu wakae wakisubiria, wamesema tusiongelee chochote mpaka pale wapelelezi watakapotupa jibu la kueleweka na kuna wengine ambao wameshakamatwa” amesema Producer S2Kizzy.

“Nimejifunza kuwa watu wajipange, ma-producer wawe na ‘back up’ ya ulinzi pia ni muhimu katika kila ofisi, nyimbo ni nyingi zimepotea tunajitahidi kutumia njia moja au nyingine vitu vyote vikae kwenye mstari”.

Tukio la kuvamiwa kwa S2Kizzy lilitokea siku ya kuamkia Oktoba 15 ambapo alifanyiwa uharibifu wa vifaa vyake vya studio na kupigwa kwa baadhi ya watu waliokuwepo ndani ya studio hiyo.

LEAVE A REPLY