S2Kizzy avamiwa studio na kupigwa

0
51

Mtayarishaji wa muziki wa Bongo Fleva, Producer S2Kizzy ameeleza kuwa amevamiwa studio kwake ya ‘pluto world’ iliyopo Sinza Lion.

Baada ya kuvamiwa studio hapo alipigwa na kufanyiwa uharibifu wa vifaa vyake na watu wanaodai wao ni walinzi shirikishi.

S2Kizzy amefahamisha hilo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ambapo ameandika kuwa

“Nimevamiwa studio, kupigwa na kufanyiwa uharibufu wa studio nzima, kuvunjiwa vifaa vya   na vitu vya studio na hawa wanaodai wao ni ‘security’ na ulinzi shirikishi, studio kulikuwa na watu ambao walipigwa kama wezi wanawake walizalilishwa ikiwemo kuvuliwa nguo, kupigwa na kufanyiwa vitendo vya kinyama”.

“Nimesikitisha na nimekatishwa sana tamaa mimi kama kijana ambaye natafuta riziki, kazi zeu tunakesha na tunahangaika lakini mwisho wa siku tunavunjwa sana moyo na vitu ambavyo havina hivi ili wala lile” ameongeza.

LEAVE A REPLY