Rugemalira na mwenzake waendelea kusota rumande

0
301

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeahirisha kesi inayowakabili mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder  Singh Sethi na  mfanyabiashara James Rugemalira wanaokabiliwa na mashtaka 12, yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababisha serikali hasara.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 22, mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya wakili wa serikali, Leornad Swai, kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Mawakili wanaomtetea mfanyabiashara Harbinder Singh Sethi wameiomba Mahakama imruhusu mteja wao akatibiwe nje ya nchi.

Kutokana na kuwa na uvimbe na Baloon tumboni hali inayomsababishia maumivu makali na kumnyima usingizi kwa wiki ya nne sasa, ombi ambalo limekataliwa na Mahakama na kuagiza atibiwe Muhimbili.

LEAVE A REPLY