Ruby amaliza tofauti na Clouds Media, nyimbo zake kuanza kupigwa

0
238

Kuna msemo unaosema Bosi anuniwi umejidhihirisha kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ruby baada ya kumuomba radhi bosi wake wa zamani, Ruge Mutahaba ili nyimbo zake ziweze kupigwa Clouds Media.

Ruby aliingia katika mgogoro wa kimaslai na uongozi wa Clouds Media mpaka kupelekea nyimbo zake kusitishwa kupigwa na kituo hicho kutokana na mgogoro huo uliodumu kwa mwaka mmoja.

Mwanamuziki huyo aliyetamba na wimbo kama vile ‘Na Yule‘ ameamua kuomba radhi uongozi wa Clouds Media baada ya kushuka kimuziki kutokana na nyimbo zake kusitishwa kupigwa na media hiyo.

Ruby ameomba radhi uongozi wa Clouds Media pamoja na mashabiki wake baada ya kushuka kimuziki wakati akiwa na tofauti na uongozi huo wa Clouds Media.

Uongozi wa Clouds Media Group walisitisha kucheza nyimbo za msanii huyo kutokana na tofauti zao, hivyo sasa nyimbo zake zinachezwa baada ya kumaliza tofauti hizo.

LEAVE A REPLY