Ruby alivyopiga shoo kali Mlimani City

0
127

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Hellen George maarufu kama Ruby ameacha historia ya aina yake kwenye tuzo za SZIFF Baada ya kupiga bonge la shoo.

Rubby alikonga nyoyo za mamia waliofika kuhudhuria hafla ya utoaji wa tuzo za Sinema Zet zilizofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Rubby ambaye alipanda kwenye jukwaa la SZIFF aliamsha shangwe la maana baada ya kutoa burudani ambayo haikuacha chembe yoyote ya shaka, achilia mbali vazi lake kali.

Mashabiki mbali mbali walishindwa kujizuia na kumimiminika stejini kwa ajili ya kumtunza ambapo anasemekana kupata pesa nyingi sana.

Lakini pia mastaa mbali mbali kama Jokate Mwegelo, Mama Diamond na wengineo wamempongeza Ruby na kuisifia sauti yake matata.

LEAVE A REPLY