Rubani afariki dunia wakati ndege ikiwa safarini

0
273

Rubani wa ndege iliyokuwa safarini kutoka Dallas kwenda Albuquerque New Mexico amefariki.

Ndege hiyo aina ya Boeng 737-800, ilikuwa imesalia karibu kilomita tatu kabla ya kutua, wakati nahodha alitangaza suala la dharura, kwa mujibu wa msemaji wa uwanja wa ndege wa Albuquerque

Shirika la American Airlines lilimtaja rubani huyo kama William “Mike” Grubbs ambaye alikuwa mmoja wa marubani.

Mwaka 2015 rubani mwingine wa shirika hilo alifariki wakati wa safari kutoka Phoenix kuelekea Boston.

Ndege hiyo ilipelekwa na rubani mweza kwa njia iliyo salama hadi uwanja wa Syracuse mjini New York.

 

LEAVE A REPLY