Roy Hodgson arithi mikoba ya Frank De boer ndani ya Crystal Palace

0
89

Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson ameteuliwa kuwa kocha wa klabu ya Crastal Palace akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Frank De boer aliyetimuliwa jana.

Kocha huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kwenye klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza.

Hodgson amerithi mikoba ya Frank de Boer ambaye ametimuliwa katika kikosi hicho cha the Eagles na kumleta Ray Lewington kuwa msaidizi.

Hodgson mwenye umri wa miaka 70 anachukua nafasi hiyo ili kuiokoa Palace yenye matokeo mabovu katika ligi kuu nchini Uingereza baada ya kucheza michezo yake minne ya ufunguzi pasipo ushindi.

Hodgson, amesema kuwa “Hiyo ni timu ya ujanani mwake na amekuwa akifuatilia mara kwa mara pindi inapocheza jambo ambalo linampa nafasi ya kukumbuka mambo mengi”, ameuwambia mtandao wa klabu hiyo.

LEAVE A REPLY