Rose Ndauka atamani mtoto wa pili

0
319

Muigizaji wa Bongo Movie, Rose Ndauka amefunguka na kusema kuwa anatamani kupata mtoto wa pili kwasasa.

Ndauka amesema kuwa anatamani sana kuongeza mtoto mwingine kutokana na raha anayoipata kutoka kwa mtoto wake huyo wa kike aitwaye Naveen lakini bado hajapata wa kuongeza naye.

Pia Rose amesema kuwa, mtoto wake amekuwa akimpa faraja sana kila wakati hivyo kumpa hamu tena ya kuongeza mtoto mwingine ili azidishe furaha aliyonayo sasa.

Rose Ndauka ameongeza kwa kusema kuwa mtoto wake huyo anamfanya azidi kupambana katika maisha kwa ajili ya kumtunza lakini kwasasa anatamani mwingine ili haweze kuishi na mwenzie ambaye kwasasa yupo peke yake.

Kutokana na kauli ya Rose kuwa ajampata wa kuzaa naye mtoto inaonesha kuwa kwasasa muigizaji huyo yupo single.

LEAVE A REPLY