Rose Ndauka ajutia enzi za ujana wake

0
99

Muigizaji wa Bongo Movie, Rose Ndauka amefunguka na kusema kipindi ambacho ametumika sana kwenye maisha yake ni pale alipokuwa kwenye umri wa ujana na ujinga “Foolish Age” ambapo alikuwa anapenda starehe kupitiliza.

Rose Ndauka amesema katika umri huo wa kijinga, ametumika sana kwa kwenda kwenye kumbi za starehe kuanzia Ijumaa hadi Jumapili.

“Muda ambao nahisi nimetumika ni ule wakati nakuwa na umri wa kijinga na ujana “Foolish Age” maana nilikuwa naenda club kuanzia Alhamisi hadi Jumapili, tena ilikuwa ni sababu ya marafiki ambao wamenizunguka ila nashukuru Mungu nimebadilika, sasa hivi naishi kwenye ndoto za maisha yangu” amesema Rose Ndauka.

Aidha Rose Ndauka amewachana wanawake ambao wanategemea kudanga ili kupata pesa kwenye maisha yao kwa kusema.

“Unaweza ukawa na sponsor “danga” kibao, lakini ukaishia kupiga picha za selfie hotelini, kula na kununua nywele lakini hautafanya kitu cha maana, ila mimi nimepambana mwenyewe hadi kufikia hapa kufungua ofisi yangu na kuajiri vijana wengine”

Rose Ndauka kwa sasa ni Mkurugenzi katika ofisi yake inayojishughulisha na masuala ya urembo.

 

LEAVE A REPLY