Rose Ndauka afunga ndoa

0
192

Muigizaji wa Bongo Movie, Rose Ndauka amefunguka na ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi mfanyabiashara ajulikanae kwa jina la Haffiyy.

Tukio hilo la wao kufunga ndoa limefanyika wikiendi hii iliyopita, ambapo ikiwa imepita mwezi mmoja na siku kadhaa tangu Rosse Ndauka alipovalishwa pete siku ya Machi 2, 2020.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Rose Ndauka ameandika,  “Allahmdulilah basi ndiyo hivyo Mrs Mkongwa tena, na ndoa inaraha yake bwana aaaaga mume wangu nakupenda.

Nae mume wake kwenye mtandao wake wa kijamii ameandika “Akhsante Allah na mimi nimepata utulivu sitochoka kukushukuru, ndoto zangu zimetimia juu ya hili jambo, naamini mengi mazuri yanakuja wewe ni kiboko yangu na kuanzia sasa eti unavimbaa kuitwa mama Mkongwa”.

Kabla ya ndoa hiyo Rose Ndauka aliwahi kuwa kwenye mahusiano na mzazi mwenziye Chiwambo Bandawe ambapo walibahatika kupata mtoto mmoja.

Rosse Ndauka anaungana na mastaa wengine wa kike ambao wapo katika ndoa kama Shilole, Mayasa Mrisho, Mboni Masimba na Shamsa Ford ambaye ameingia na ametoka kwenye ndoa.

LEAVE A REPLY