Rosa Ree awapa ushauri wanawake wenzie

0
296

Mwanamuziki wa Hip Hop nchini, Rosa Ree ameibuka na kuwataka wanawake wasihukumu wanaume wote kwenye mahusiano sababu waliumizwa na mwanaume mmoja, badala yake wawape nafasi.

Rosa Ree ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha PlanetBongo cha East Africa Radio, kinachoruka kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 7 Mchana hadi saa 10 kamili jioni.

Rosa Ree amesema kuwa “mwanamke ukitongozwa na Mwinyi, usijekusema eti wanaume wote ni Majibwa sababu JR alikuumiza, mkubalie tu, usimuhukumu mtu sababu ya makosa ya watu wengine”

Kuhusiana na hukumu yake BASATA Rosaree amesema alilazimika kukata rufaa ili aweze kufanya sanaa kama kawaida na kwa sasa yupo kwenye uangalizi wa miezi 6

“Nilikata rufaa kwa Waziri Mwakyembe, na akanisikiliza na wamenipa uangalizi wa miezi 6, nashukuru sana, ila pia BASATA nililipishwa faini ya Milioni 2” amesema Rosaree

 

LEAVE A REPLY