Rosa Ree akanusha kutoka kimapenzi na Young Dee

0
304

Mwanamuziki wa rap Bongo, Rosa Ree amekanusha kutoka tetesi za kutoka kimapenzi na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Young Dee.

Rosa Ree amesema kuwa watu wamekuwa wakizusha mambo hasa wanapoona watu wamekuwa na ukaribu hata kama ni wa kibiashara na kikazi.

Young Dee
Young Dee

Mwanamuziki huyo pia amesema kuwa kwa muda sasa amekuwa singo bila kujiingiza katika mahusiano yoyote na ikitokea siku akiwa katika mahusinoa yaliyo serious basi  lazima atawatambulisha mwanaume  lakini sio kupitia katika kurasa za udaku kama inavyotokea saa hivi kwa young dee.

Wasanii wengi wamekuwa wakiambiwa au kuhisiwa kuwa wanatoka na wasanii wenzao lakini wanakuwa wanakanusha lakini ukweli wanaokuwa nao wenyewe na mbaya zaidi mambo yanapokuwa magumu ndio siri zinaanza kuvuja na kushindwa kuyatatua matatizo yao ingawa sio vizuri kuonyesha mahusiano yao katika mitandao.

LEAVE A REPLY