Rosa Ree afunguka kuhusu mafaniko yake

0
397

Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Rosa Ree amefunguka na kusema kuwa kujituma kwake ndiyo kumesababisha kupata menejimenti kutoka nchini Afrika Kusini.

Rosa Ree amesema hayo baada ya wiki iliyopita kupata dili na kampuni moja kutoka nchini Afrika Kusini ambapo pia amepewa nyumba la milioni 400.

Amesema kuwa  “Ukiwasikiliza wanamuziki wa kike wa Bongo, wengi wanavyorap ni ‘local’ ndiyo maana hata hawatusui kama mimi, kikubwa aina yangu ya uimbaji inanifanya kupata mashabiki wengi zaidi nje ya Bango,”.

Mwanamuziki huyo amepata menejimenti kutoka nchini Afrika Kusini ambapo inaitwa kwa jina la Dimo Production.

Rosa Ree alisema kuwa, siri hiyo ni namna ya uimbaji wake kwani haujakaa Kibongo sana na anajiweka ‘kimtoni’ zaidi ndiyo maana anafanikiwa.

LEAVE A REPLY